Matthew 5:38-48

Kuhusu Kulipiza Kisasi

(Luka 6:29-30)

38 a “Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Jicho kwa jicho na jino kwa jino.’ 39 bLakini mimi nawaambia, msishindane na mtu mwovu. Lakini kama mtu akikupiga kwenye shavu la kuume, mgeuzie na la pili pia. 40 cKama mtu akitaka kukushtaki na kuchukua joho lako, mwachie achukue na koti pia. 41 dKama mtu akikulazimisha kwenda maili moja, nenda naye maili mbili. 42 eMpe yeye akuombaye, wala usimgeuzie kisogo yeye atakaye kukukopa.

Upendo Kwa Adui

(Luka 6:27-28, 32-36)

43 f “Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Mpende jirani yako na umchukie adui yako.’ 44 gLakini ninawaambia: Wapendeni adui zenu na waombeeni wanaowatesa ninyi, 45 hili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana yeye huwaangazia jua lake watu waovu na watu wema, naye huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. 46 iKama mkiwapenda tu wale wanaowapenda, mtapata thawabu gani? Je, hata watoza ushuru hawafanyi hivyo? 47Nanyi kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, je, mnafanya nini zaidi ya wengine? Je, hata watu wasiomjua Mungu, hawafanyi hivyo? 48 jKwa hiyo kuweni wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Copyright information for SwhNEN